• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

Historia

Mkoa wa Shinyanga ulikuwa ni sehemu ya Mkoa wa Ziwa (Lake Province) mpaka mwaka 1963 ulipoanzishwa rasmi ukiwa na Wilaya tatu (3) ambazo ni Maswa, Shinyanga na Kahama iliyomegwa kutoka Mkoa wa Tabora. Kuanzia Mwaka 1972 hadi mwaka 1982 Serikali ya Mkoa ilikuwa katika mfumo wa Madaraka Mikoani ambapo vyama vya ushirika, utemi na Serikali za Mitaa zilifutwa. Mkoa uliongozwa na Mkuu wa Mkoa, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Mkoa (Regional Development Director) ambaye alisimamia wakuu wa idara mbalimbali. Muundo huu wa utawala ulitumika hadi mwaka 1997 ambapo ulibadilishwa kwa mujibu wa Sheria ya Tawala za Mikoa (Regional Administration Act No. 19 of 1997). Sheria hiyo ilifuta cheo cha Mkurugenzi wa Maendeleo wa Mkoa na kuanzisha cheo cha Katibu Tawala Mkoa. Katibu Tawala Mkoa ndiye Mtendaji Mkuu wa shughuli za Serikali katika Mkoa.

Mkoa wa Shinyanga uliendelea kukua ambapo maeneo mapya ya Utawala yalianzishwa na kufikia Wilaya saba ambazo ni Kahama, Bukombe, Maswa, Kishapu, Bariadi, Meatu na Shinyanga. Aidha kuanzia mwaka 2012 kutokana na Mkoa kukidhi vigezo muhimu vya kitaifa vya uanzishaji maeneo mapya ya utawala, Serikali  ilifanya uamuzi wa kuanzisha maeneo mapya ya Utawala ambapo Mikoa mipya ya Simiyu na Geita ilianzishwa ikiwa imemega baadhi ya Wilaya za Mkoa wa Shinyanga. Wilaya za Bariadi, Maswa na Meatu zilimegwa kuanzisha Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Bukombe ilipelekwa Mkoa mpya wa Geita. Aidha, Mkoa wa Shinyanga uliongeza maeneo ya Kiutawala kwa kuanzisha Halmashauri mpya za Kahama mji mwaka 2012, Msalala na Ushetu mwaka 2013 ambazo zilitokana na kugawanywa kwa Wilaya ya Kahama. Uamuzi huu wa Serikali unalenga kuboresha huduma za kiutawala na maendeleo ili wananchi waweze kuzipata kwa karibu zaidi. Jedwali lifuatalo linaloonesha Mgawanyo wa Mkoa kiutawala kwa sasa.

 

Mgawanyo wa Mkoa wa Shinyanga Kiutawala


 
Wilaya
 
Halmashauri 
Ukubwa wa eneo (km2)
 
Tarafa 
 
Kata 
 
Vijiji 
 
Mitaa 
1
Kahama
1
Manispaa ya Kahama

1,515

2

20

45

32

2
Ushetu

5,311

2

20

112

-

3
Msalala

2,637

1

18

92

-

2
Kishapu
4
Kishapu

4,334

3

25

117

-

3
Shinyanga
5
Shinyanga

4,212

3

26

126

-

6
Manispaa ya Shinyanga

548

3

17

19

55

Jumla

18,555

14

126

511

87


Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Machi 2017

Mipaka ya Mkoa:

Mkoa wa Shinyanga uko Kaskazini – Magharibi mwa Tanzania na Kusini mwa Ziwa Victoria.  Mkoa unapakana na Mikoa ya Mwanza, Simiyu na Geita kwa upande wa Kaskazini, upande wa Mashariki Mkoa wa Simiyu, Upande wa Magharibi Mkoa wa Geita upande wa Kusini Mkoa wa Tabora. Mkoa uko kati ya nyuzi za Latitudo 30 12’ - 40 27’ Kusini mwa Ikweta na nyuzi za Longitudo  310 29’ - 340 18’ Mashariki ya Greenwich. Mkoa wa Shinyanga una eneo la kilometa za mraba 18,555..

RAMANI YA MKOA WA SHINYANGA KIUTAWALA


Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Shinyanga, Machi, 2017

3.0.1 UONGOZI WA MKOA

Mkoa wa Shinyanga umeongozwa na wakuu wa mikoa 24 tangu mwaka 1963 kama orodha inavyoonesha hapa chini:


Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA MAPITIO YA ROBO MWAKA KWA KIPINDI CHA OKT - DES 2024 CHA (PJT MMMAM) CHAFANYIKA MKOANI SHINYANGA.

    February 28, 2025
  • RCC SHINYANGA YARIDHIA MAPENDEKEZO NANE (8) YA MATUMIZI BORA YA ARDHI.

    February 27, 2025
  • KUKAMILISHWA KWA MIRADI YA BARABARA KUTAPUNGUZA KERO KWA WANANCHI – RC MACHA

    February 26, 2025
  • WALIMU, TOENI ELIMU INAYOENDANA NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA -RC MACHA

    February 24, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa