Uzinduzi wa chanjo mpya ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi itafanyika tarehe 23 Aprili, 2018. Katika Mkoa wa Shinyanga uzinduzi huo utafanyika katika viwanja vya zimamoto eneo la Nguzo nane kuanzia saa 2.00 asubuhi.
Baada ya uzinduzi, chanzo hiyo itaendelea kutolewa katika vituo vyote vya kutolea huduma ya afya na katika shule zote za msingi na sekondari.
Walengwa wa chanjo hii ni wasichana wenye umri wa miaka 14.
Wazazi na walezi wenye watoto wa kike wa umri wa miaka 14 wawapeleke watoto wao wakapate chanjo hiyo ili kuwakinga na saratani ya mlango wa kizazi hapo baadaye.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack.
"JAMII ILIYOPATA CHANJO NI JAMII YENYE AFYA, TIMIZA WAJIBU WAKO"
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa