Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), atafanya ziara ya kikazi Mkoani Shinyanga kuanzia tarehe 07 – 11 Julai, 2018, katika Halmashauri zote sita (6) za Mkoa wetu.
Lengo la ziara hii ni kuhamasisha na kufuatilia utekelezaji wa shughuli za maendeleo pamoja na kukagua masoko ya pamba.
Pamoja na shughuli hizo, Mheshimiwa Waziri Mkuu atazungumza na wananchi na watumishi wa Umma kwa kila Halmashauri.
Aidha, tarehe 10 Julai, 2018 Mheshimiwa Waziri Mkuu atakuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mpango wa Bima ya Afya kwa wakulima kupitia vyama vya Ushirika ambao Kitaifa utafanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, Wilayani Kahama.
Wananchi wote wa Mkoa wa Shinyanga mnaombwa kujitokeza kwa wingi kumpokea Mheshimiwa Waziri Mkuu atakapopita katika maeneo yenu.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa