Ufugaji Mkoa wa Shinyanga
Uchumi wa Mkoa umeendelea kutegemea kilimo na ufugaji.
Mifugo inayofugwa ni pamoja na ng’ombe, mbuzi, kondoo, punda, nguruwe na kuku.
Mkoa wa Shinyanga unakadiriwa kuwa na ng’ombe 1,221,784, mbuzi 757,772, kondoo 372,351, nguruwe 24,558 na punda 19,460.
Idadi ya kuku wa asili inafikia 2,081,006, kuku wa mayai 216,980 na kuku wa nyama wako 10,729.
Idadi kubwa ya mifugo inayofugwa katika Mkoa wa Shinyanga ni ya asili.
Mauzo ya ng’ombe hai yanaongoza kwa kuwapatia wafugaji fedha nyingi yakifuatiwa na mauzo ya mbuzi.
Serikali kuu ilikusanya maduhuli yanayotokana na ushuru na usafirishaji wa mifugo jumla ya shilingi 319,230,000 sawa na asilimia 90.61 ya malengo ya mwaka 2015/2016.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa