Shinyanga kuna vivutio vya utamaduni, kuna Mapango yaliyotumika kupumzishia Watumwa enzi za biashara ya utumwa yanaitwa mapango ya Ngaganulwa yapo Usanda Shinyanga, kuna makumbusho ya Chifu Mwana Malundi ambayo yanapatikana Kishapu, kuna Kisima cha ajabu kischo kauka juu ya mwamba kilichopo Kishapu, kuna maporomoko ya maji yako Wilaya ya Msalala,kuna makaburi ya pamoja la bibi na Bwana la Machifu, kivutio cha Mahakama ya Kichifu eneo la Iselamagazi Halmashauri ya Shinyanga, kuna kivutio cha Chemchem ya maji moto UzogoleShinyanga, kisima cha maajabu Salawe, maajabu ya Kisima hiki tangu dunia iumbwe kisima hicho maji yake hayajawahi kujaa wala kupugua.
OFISI YA MKUU WA MKOA, MKOA WA SHINYANGA, 04 MTAA WA BOMA
Anuani: P.O.Box 320, 37180,SHINYANGA, TANZANIA
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa