Tuesday 30th, May 2023
@Nyakabindi, Bariadi
Sikukuu ya wakulima inayofahamika kuwa Nanenane ina sherekewa nchini kote tarehe 8 Agosti kila mwaka. Sherehe hiyo inatayarishwa na kuratibiwa na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kwa kushirikiana na Shirika la Chama cha Kilimo Tanzania (TASO) na kuhusisha Taasisi, Wizara na mtu mmoja mmoja wanaoshughulika na kilimo.
Miaka iliyopita sherehe hizi zilikuwa zikifanywa tarehe saba Julai kila mwaka na kuzingatia mafanikio makubwa na changamoto zinazokabili sekta ya kilimo inayowashirikisha wadau wote kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa.
Maadhimisho haya husherehekewa katika ngazi ya kanda ambapo kanda ya Ziwa Mashariki ambayo ni Mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga, yatafanyika katika Uwanja wa Nyakabindi Bariadi, Mkoani Simiyu.
Kauli Mbiu ya maadhimisho haya ni WEKEZA KATIKA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KWA MAENDELEO YA VIWANDA.
Mgeni Rasmi siku ya ufunguzi rasmi wa maadhimisho tarehe 01 Agosti, 2018 ni Mhe. Samia Suluhu Hassani, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli atakuwa mgeni rasmi siku ya kilele cha maadhimisho tarehe 08/08/2018.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa