• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

AKINA MAMA NA WASICHANA, JITOKEZENI KUSHIRIKI FURSA ZA KIUCHUMI - RC MACHA

Posted on: March 6th, 2025

Na. Paul Kasembo, MSALALA DC.

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewasihi wanawake na wasichana mkoani Shinyanga kujitokeza kwa wingi kushiriki katika fursa mbalimbali za kiuchumi na ujasiriamali zinazojitokeza ili kujiimarisha kiuchumi.

RC Macha ameyasema haya Machi 6, 2025 kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika Kata ya Bugarama, Halmashauri ya Msalala Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga na kuhudhuriwa na Viongozi wa Taasisi za Serikali na Binafsi,Watumishi  pamoja na wanachi, maadhimisho yenye Kaulimbiu “Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji”.

“NIchukue fursa hii kuwahimiza wanawake na wasichana wote kujitokeza kushiriki katika fursa mbalimbali za kiuchumi na ujasiriamali  zinazojitokeza ili kujiimarisha kiuchumi”, amesema RC Macha.

Aidha RC Macha ameongeza kwa kuwasihi wananawake kutumia nishati safi ya gesi na umeme ili kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuifanya Tanzania iwe na matumizi ya nishati safi na utunzaji wa mazingira.

Akiwasilisha taarifa fupi ya shughuli zilizofanyika kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake kwa siku 3, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga Bi. Rehema Edson amesema kuwa wamefanikiwa kushirikiana na wajasiriamali 15, Taasisi takribani 9 zimeshiriki maonesho na kutoa huduma, zoezi la ugawaji miti ili kutunza mazingira pamoja na kongamano kubwa la wanawake ambapo takribani 466 walihudhuria na kupata elimu ya masuala mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi mkoani Shinyanga Dkt. Regina Malima ameshauri kuanzishwa kwa sera na mikakati ya kuwakwamua wanawake na wasichana kiuchumi sambamba na utoaji elimu endelevu ili wafahamu fursa zilizopo za kuwawezesha kiuchumi.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake mkoani Shinyanga yamehitimishwa na RC  Macha ambaye ndiye mgeni rasmi ambapo yaliambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo maandamano, kutembelea mabanda ya maonesho pamoja na utoaji hundi za mikopo ya Serikali ya asilimia 10 kwa vikundi vya wajasiliamali.

Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • RC MHITA AWAHAMASISHA WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI MKOANI SHINYANGA

    November 13, 2025
  • RC MHITA AKUTANA NA MSANII BANDO MC, APONGEZA JUHUDI ZA KUSAIDIA VIJANA SHINYANGA

    November 11, 2025
  • RC MHITA APONGEZA UONGOZI MPYA WA KANISA LA WASABATO NGBF MKOANI SHINYANGA.

    November 07, 2025
  • WANAFUNZI 29,193 KUFANYA MTIHANI WA UPIMAJI KIDATO CHA PILI SHINYANGA.

    November 07, 2025
  • Angalia zote

Video

RC MHITA AWAHAMASISHA WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI MKOANI SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    OFISI YA MKUU WA MKOA, MKOA WA SHINYANGA, 04 MTAA WA BOMA

    Anuani: P.O.Box 320, 37180,SHINYANGA, TANZANIA

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa