Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack jana tarehe 26/06/2019 katika uwanja wa Majengo, Wilayani Kahama wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya hiyo na kusikiliza kero zao.
Katika mkutano huo, Mhe. Telack amewaeleza wananchi utekelezaji wa mambo mbalimbali yanayofanywa na Serikali ya Mkoa katika kuwasogezea huduma karibu ikiwemo ujenzi wa vituo 11 vya afya, Hospitali 2 za Wilaya, ujenzi wa Ofisi za Maafisa Tarafa na nyumba za watumishi wa jeshi la Polisi.
Telack amesema iwapo wananchi watakuwa na huduma karibu hasa afya, wataweza kufanya kazi zao kwa uhuru na amani.
Aidha, amewataka wananchi wa Wilaya ya Kahama kutowasikiliza watu wanaochochea migogoro na kuandika maneno yasiyo ya ukweli kwenye magazeti.
"Kuna baraza la wazee linalotambulika kisheria, kazi yake ni kuishauri Serikali na siyo vinginevyo,hivyo wananchi msiwasikilize hao wengine" amesisitiza Telack.
Mmoja wa wananchi wa Wilaya ya Kahama, Mzee Ndali akitoa kero yake kwa Mhe. Mkuu wa Mkoa hapo jana katika uwanja wa Majengo, Kahama.
Diwani wa kata ya Majengo Kahama, akiwasilisha kero za kata hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga jana, katika uwanja wa Majengo, Kahama
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Majengo Kahama,wakifuatilia majibu ya kero zao.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa