Na. Paul Kasembo, Msalala.
BARAZA la Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala limempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri Ndugu Khamis Katimba kwa kazi nzuri anayoifanya tangu kuteuliwa kwake na kuanza kuitumikia Msalala hususani katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ukusanyaji wa mapato, ustawi wa wananchi na uboreshaji wa utawala bora kwa Wanamsalala.
Pongezi hizi zimetolewa kwa niaba ya Baraza leo tarehe 8 Mei, 2024 na Mhe. Shija Joseph Luyobya ambaye ni Diwani wa Kata ya Bulyanhulu katika Baraza la robo ya tatu Januari - Machi 2023/2024 ambalo pamoja na mambo mengine lilipokea na kujadili taarifa kutoka kwa Kamati mbalimbali za Kudumu ambapo wajumbe wa Baraza walimpongeza kwa dhati huku likionesha kuvutiwa zaidi na ubunifu wake katika utendaji kazi wake.
"Mhe. Mwenyekiti, sisi Waheshimiwa Madiwani kwa dhati kabisa tunampongeza sana Mkurugenzi Mtendaji wetu wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala kwa utendaji bora wake katila kuwahudumia wananchi, kutekeleza miradi ya maendeleo, kuboresha utawala bora, upatikanaji wa Hati Safu na kubwa zaidi kuongeza na kuboresha kiwango cha ukusanyaji wa mapato ambapo mpaka sasa amekusanya 98% wakiwa wamevuka lengo la serikali kabla ya Juni 30, 2024," amesema Mhe. Luyobya.
Kando na pongezi hizi, Baraza la Madiwani limeipongeza sana Mhandisi Maduhu Magili ambaye ni Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kahama kwa namna ambavyo wanatekeleza miradi yao ambayo imekuwa na tija zaidi kwa wananchi wa Msalala.
Kwa upande wa TARURA Wilaya wajumbe wameshauri Eng. Ally Ndumbalo ambaye ni Kaimu Meneja Wilaya ya Kahama waanze na vipolo (miradi isiyokamilika) ambavyo vipo kabla hawajaanza utekelezaji wa miradi mipya kwa mwaka 2024/2025 ili kupunguza maswali kwa wananchi ukizingatia mwaka huu ni wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa