BARICK BULYANHULU YAZINDUA KAMPENI YA ZERO MALARIA
Katika kuunga mkono Juhudi za Serikali katika kukabiliana na Ugonjwa wa Malaria Mgodi wa Barick Bulyanhulu unaopatikana Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga umezindua kampeni ya Kuhamasisha Jamii kujinga na ugonjwa huo kampeni Ijulikanayo ZERO MALARIA INAANZA NA MIMI ,WEWE NA SISI SOTE.
Akizungumza katika uzinduzi huo iliofanyika katika kata ya Bugarama Meneja wa Mgodi wa Bulyanhulu CHEICK SANGARE Amesema Barick Imekuwa ikishirikiana na serikali katika mambo mbalimbali lakini kwa sasa tutaihamasisha jamii kujikinga na ugonjwa malaria ili kupunguza vifo hasa vya mama na watoto ambao wamekuwa wahanga wa ugonjwa huu.
Aidha amesema kupitia kampeni hii kaya zipatazo Elfu 17,500 na watu Zaidi ya Elfu 5000 watanufaika ambapo watapata nafasi ya kupata vyadarua pamoja na kunyunyuziwa dawa makazi yao.
Akitoa salamu kwa niaba ya serikali Mkurugenzi Halimashauri ya msalala KHAMIS KATIMBA ameupongeza mgodi wa Barick Bulyanhulu kwa kuzindua kampeni hiyo ambapo amewaomba wananchi wataofikiwa na kampeni hiyo kuwa ushrikiano watoa huduma watakaofika katika kaya zao.
Akitoa tathimini ya maambukizi ya ugonjwa huo katika kata mbili ya bugarama na bulyanhulu Dkt. Martin Mazigwa Ambae ni Mratibu wa malaria amesema kiwango cha maambukizi kimepungua mambapo mwaka 2020-2023 kutoka asilimia 29.4 hadi Asilimia 18.9 katika kaa hizo mbili.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa