Na. Shinyanga RS.
BI. Christina Solomon Mndeme ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) amekabidhi rasmi Ofisi kwa Mkuu mpya wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha huku akimtakia kila lenye kheri katika kuwatumikia Wanashinyanga na Watanzania kwa ujumla.
Makabidhiano haya yamefanyika tarehe 18 Machi, 2024 katika jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambapo yalihudhuriwa na vingozi mbalimbali wakiwemo wa Kamati ya Usalama.
Akizungumza mara baada ya makabidhiano, Mhe. Macha amesema kuwa, anamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa uzima na afya, kipekee anamshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwa na imani nae na hata amemteuwa tena katika nafasi hii mpya ili aendelee kumsaidia kazi kwa Mkoa wa Shinyanga.
Aidha amesema kuwa, ataendelea kuwatumikia Wanashinyanga kuanzia pale alipoishia Bi. Christina, na ataendelea na juhudi zaidi na maarifa katika kuwatumikia wqnanchi na kuhakikisha kuwa wanakuwa na maendeleo, afya na ustawi wa kijamii.
Mhe. Macha anakuja kuchukua nafasi ya Bi. Christina ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu - Mazingira kufuatia mabadiliko yaliyofanywa na Mhe. Rais ambapo Mhe. Macha anatikea kwenye nafasi ya Naibu Katibu Mkuu CCM Bara.
HABARI PICHA NA MATUKIO
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa