KAHAMA.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba Mapema leo tarehe 4 Desemba, 2024 akiwa ameambatana na mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama @mboni_mhita na viongozi wengine ameshiriki hafla ya Utiaji Saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Stendi Kuu ya Mabasi eneo la Mbulu kwenye Manispaa ya Kahama, Ujenzi wa Soko kuu la Sango, Uboreshaji wa kituo kidogo cha Mabasi Pamoja na Soko la Wajasiriamali eneo la Zongomela.
Mkataba huo ni baina ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama na Mkandarasi M/s SIHOTECH Engineering Company Ltd. na AMJ Global Multi Contractors Company Ltd na Gharama ya Mkataba huo ni TZS 27,439,647,165.13 ambapo Muda wa utekelezaji wake ni Miezi 12 kuanzia tarehe 15 Desemba, 2024 hadi tarehe 14 Disemba, 2025.
Hafla hiyo imefanyika Mapema leo kwenye eneo litakalotekelezwa mradi huo Mtaa wa Mbulu, kata ya Mhongolo kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Kahama.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa