Na.Paul Kasembo, TINDE.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Anamringi Macha ameishukuru Serikali ya Awamu ya 6 inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi cha fedha takribani Bilioni 846 ndani ya miaka 3 kwa ajiri ya kuboresha shughuli za kiuchumi na kijamii mkoani Shinyanga ambapo hivi sasa takribani vijiji vyote 506 na mitaa yote imefikiwa kwa miradi tofauti tofauri ikiwemo ya afya, elimu, miundombinu, maji, umeme uwezeshaji wananchi kiuchumi nk.
RC Macha ameyasema haya leo tarehe 9 Oktoba 2024 akiwa kwenye ziara ya Katibu Mkuu CCM Balozi. Dkt. Emmanuel Nchinbi kwenye Kata ya Tinde iliyopo Wilaya ya Shinyanga huku akimpongeza sana Dkt. Nchimbi kwa kazi nzuri anazozifanya.
“Naishukuru sana Serikali ya Awamu ya 6 inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia kiasi cha fedha takribani Bil. 846 ndani ya miaka hii 3 kwa ajiri ya kuboresha shughuli za kiuchumi na kijamii, nasi hatuna budi kuendelea kuhakikisha fedha hizi zinatumika kama zilivyopangwa kwa maendeleo ya wananchi wa Mkoa wetu,” amesema RC Macha.
Akizungumza na Wananchi wa Kata Balozi Dkt. Nchimbi amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Macha kuendelea kutatua changamoto na kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Kata ya Tinde na Mkoa kwa ujumla ili kuhakikisha wanaenda sambamba na kasi ya ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuleta maendeleo.
Dkt. Nchimbi akiwa ameambata na Sekretarieti ya CCM Taifa atafanya ziara ya siku 3 katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Kahama Manispaa na mwisho Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ili kuimarisha Chama cha Mapinduzi, kuangalia utekelezaji wa ilani ya Chama pamoja na kupokea, kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa