Na Shinyanga RC.
MKUU Wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita ameipongeza Halmashauri ya Msalala kwa jitihada zake mbalimbali zinazofanywa zikiwa na lengo la kutimiza ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) lengo likiwa ni kuleta maendeleo kwa Wilaya na taifa kwa ujumla.
Pongezi hizo zimetolewa leo katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Msalala wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Waheshimiwa Madiwani na wakuu Divisheni na Vitengo wa Msalala ambapo pia amemshukuru Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme kwa kukubali ombi la kutoa wakufunzi wawili kuwezesha mafunzo hayo.
Mafunzo haya ni yenye kuongeza ufanisi katika kusimamia miradi ya maendeleo ndani ya mamlaka wanazoziongoza kwani Mheshimiwa Diwani ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kata na ikumbukwe Serikali ya awamu ya sita inapeleka fedha nyingi Katani hivyo mafunzo haya yataongeza maarifa zaidi katika kusimamia miradi hiyo.
Kwa upande wao Waheshimiwa Madiwani wamemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi ndani ya Halmashauri Ili kuhakikisha jamii inaimarika kwa kuwa na huduma za msingi ikiwemo Afya, Elimu, Maji, Barabara na Nishati ya Umeme vijijini kupitia mradi wa REA na kumwomba Mkuu wa Wilaya Mhe. Mboni Mhita kufikisha salamu za Baraza kwa Mhe. Rais na kuahidi kusimamia miradi yote kwa ufasaha.
Sambamba na hilo Baraza limewapongeza Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Mibako Mabubu na Mkurugenzi Mtendaji (W) ndg. Khamis Katimba kwa kuwezesha mafunzo haya ambayo yamelenga viongozi hawa kujua mipango ya bajeti Halmashauri inayopanga na hivyo kuwa rahisi kwao kufanya ufuatiliaji katika ngazi mbalimbali ikiwemo Halmashauri na Serikali Kuu.
Nae Katibu Tawala (W) ndg. Mohamed Mbega amewataka viongozi hao kufanya kazi zao kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni ili kulinda heshima na maadili ya uongozi.
Kwa upande wao Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) wamewaomba viongozi hao kutoa ushirikiano Kwa maafisa wa Taasisi hiyo kwani wana mpango wa kutembelea Kata zote kwa ajili ya kuanzisha Huduma ya Takukuru Rafiki yenye lengo la kuongeza uwajibikaji na utoaji huduma bora kwa jamii na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi moja kwa moja.
Sehemu ya muonekano wa wajujbe wa mafunzo wakiwa ukumbini
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa