DC MBONI MHITA AKABIDHI VITAMBULISHO VYA NIDA
Na. Paul Kasembo - USHETU
MKUU wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita amekabidhi Vitambulisho vya Urai kwa wananchi wa Halmashauri ya Ushetu huku akiwasisitiza kuvitunza ili viweze kuwakwamua katika mahitaji yao mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo kumuwekea dhamana ndugu au jamaa, kusajili laini nk.
Mhe. Mboni amekabidhi vitambulisho hivi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Nyamilangano ambapo pamoja na mambo mengine, Mhe. Mboni amepokea, kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Utatuzi wa migogoro na ufumbuzi wa kero za wananchi kupitia mikutano ya hadhara, ni utaratibu ambao amekuwa akiutumia Mhe. Mboni Mhita ambapo umeonesha matokeo chanya zaidi, kwani amekuwa akikutana na walengwa moja kwa moja ambapo hoja zao hutolewa ufafanuzi na ufumbuzi kupitia wataalam wa Halmashauri husika na jambo ambalo lipo juu yao amekuwa akishughulika nalo yeye mwenyewe.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa