Na. Shinyanga RS.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi amewataka vijana kulibeba Taifa katika mioyoni yao na siyo midomoni mwao kama ambavyo imekuwa ikionekana kwa baadhi ya vijana ikiwa ni sehemu ya kuendelea kuwaenzi Mashujaa wetu waliojitoa kulipiginia Taifa letu.
Hayo yametamkwa leo tarehe 25 Julai, 2023 wakati wa kuadhimisha Sherehe hizi ambapo alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme katika Viwanja vya Mazingira Center Manispaa ya Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, viongozi wa dini, wananchi na watumishi kutoka taasisi mbalimbali.
"Niwatake vijana wote kulibeba Taifa letu mioyoni mwetu na siyo midomoni kama ambavyo imekuwa ikionekana kwa baadhi ya vijana wenzetu ili tuweze kuendelea kuwaenzi Mashujaa wetu kwa kulilinda na kulipigania wakati wote," akisema Mhe. Johari.
Tanzania huadhimisha Siku ya Kuwakumbuka Mashujaa waliopoteza maisha yao wakiutetea, kuupigania na kuulinda Uhuru wa Tanzania kila ifikapo Julai 25, ya kila mwaka .
Siku hii ya kuwakumbuka mashujaa huambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo kufanya dua na sala maalumu kutoka kwa viongozi wa dini ya kuwaombea mashujaa hao waliopoteza maisha na kuiombea amani nchi yetu pia hufanyika Gwaride maalumu kutoka kwa vikosi vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kuwaenzi mashujaa wetu.
@christinamndeme18 @johari_samizi @shinyanga_press_club @shinyanga_tanzania

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (mwenye Gauni) akiwa na baadhi ya viongozi wa vikosi vya ulinzi na usalama alipomuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme kwenye maadhimisho ya siku ya mashujaa katika viwanja vya Mazingira Center Manispaa ya Shinyanga

Mstahiki Meya Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumhuko akipokea zana za jadi ikiwa ni ishara ya kuwaenzi mashujaa waliotumia silaha hizo katika mapambano yao wakati kupigania uhuru

Picha ikionesha sehemu ya viongozi walioshiriki katika maadhimisho ya siku ya mashujaa
OFISI YA MKUU WA MKOA, MKOA WA SHINYANGA, 04 MTAA WA BOMA
Anuani: P.O.Box 320, 37180,SHINYANGA, TANZANIA
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa