Na. Shinyanga RS.
Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI ( ELIMU ) Dkt. Charles Msonde leo tarehe 6 Oktoba, 2023 amekukagua na kutembelea utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Sekta ya elimu Manispaa ya Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengi laiini amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi huu wa shule mpya ya sekondari Ngokolo B, sekondari ya Shinyanga Wasichana na Sekondari ya Old Shinyanga
Akiongea na viongozi, watalaam na wanafunzi kwa nyakati tofauti Dkt. Msonde amesema kuwa ameridhishwa sana na utekelezaji wa miradi hii huku akiwataka mafundi wanaojenga kuongeza kasi ya ujenzi, wazingatie viwango vya bora na thamani ya fedha ili yaweze kuwanufaisha na vizazi vijavyo.
"Nawapongeza sana kwa utekelezaji wa miradi hii, nimeridhishwa na kasi ya ujenzi huu, lakini niwaombe mafundi mzingatie ubora, muda uliopangwa na uimara wa majengo kwa kuzingatia thamani ya fedha iliyotolewa na Serikali ili iwanufaishe na vizazi vijavyo," alisema Dkt. Msonde.
Katika ziara hii pia aliambatana na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo pamoja na wataalam mbalimbali kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Manispaa ya Shinyanga.
Katika hatua nyingine Dkt. Msonde amewataka wananfuzi wa shule hizi kusoma kwa bidii kwakuwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekwisha wawekea mazigira bora, rafiki na salama kabisa ya wao kupata elimu, shukurani zao wanafunzi kwa Mhe. Rais ni kusoma kwa bidii ili waweze kufikia malengo yao.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa