DKT. SENGATI AHAIDI KUPAMBANA NA CHANGAMOTO YA UMASIKINI SHINYANGA
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati amesema Mkoa wa Shinyanga ni Mkoa wenye utajiri wa rasilimali lakini hali ya maisha ya wananchi Mkoani humo haiendani rasilimali zilizopo katika mkoa huo akiitaja hiyo kuwa changamoto kubwa ya mkoa wa Shinyanga.
Dkt. Sengati amesema hayo leo wakati wakati wa kumkaribisha Katibu Tawala Mpya wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Batlida Buriani ambaye kwa mara ya kwanza amefika katika ofisi yake mpya tayari kwa makabidhiano ya ofisi na kuendelea majukumu yake mapya.
Dkt. Sengati aliongeza kuwa Shinyanga kuna umasikini ambao umejificha katika utajili mkubwa lakini hususani kwa wakazi wa pembezoni akihaidi kuifanyia kazi changamoto hiyo ili wakazia wa mkoa wa Shinyanga waweze kuinua hali yao itakayoendana na rasilinmali zilizopo.
‘’Unakuta mtu ana ngombe zaidi ya elfu moja lakini mtu huyo anaishi katika mazingira yaliyoduni sana au haoni faida ya kupeleka mtoto katika elimu ya juu hii changamoto ambayo lazima tuifanyie kazi”. Alisisitiza Dr. Philemon Sengati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Naye Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Dkt. Batlida Buriani amesema kuwa lazima kuwe na ubunifu katika kutafuta vyanzo vipya vya mapato na kuzitaka Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga kukusanya mapato bila ya kuleta kero kwa wananchi.
Aidha Dkt. Buriani amesema pia ipo aja ya kuingalia upya mianya yote ambayo imekuwa ikichangia upoteaji wa mapato kwa lengo la kuinua na kukuza uchumi wa mkoa wa Shinyanga.
Pamoja na mambo mengine Dkt.Buriani amesema ataliangazia pia sula la maendeleo na ustawi wa jamii kwa kuhakikisha ipo miradi ambayo inaweze kuingiza kipato kwa wazee na wanawake ili nao waweze kuchangia katika kujiletea maendeleo lakini pia kuchangia katika maendeleo ya Taifa.
‘’Najua Shinyanga kuna wazee wengi sana na hali zao sio nzuri na katika jambo ambalo ninataka tufanikiwe ni kuhakikisha wanashiriki katika miradi ambayo itawanufaisha najua kuwa Shinyanga kuna mifugo mingi hivyo tunaweza tukatumia fursa ya mifugo iliyopo kuzalisha siagi kwa wingi sana.’’Alisema Dkt. Batlida Buriani Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga.
Naye aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bw. Albert Msovera alisema Mkoa wa Shinyanga bado una chanagamoto ya watumishi lakini zipo juhudi ambazo zimekuwa zikiendelea kuhakikisha changamoto hiyo inatatuliwa na hivyo kumtaka mrithi wake kuangalia namna bora ya kuendelea kulifanyia kazi jambo hilo ili kukabiliana na upungufu wa rasilimali watu.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa