• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

GARI HII HILI LISIGEUZWE KUWA DALADALA – RC MACHA

Posted on: March 3rd, 2025

Na. Paul Kasembo, SEGESE - MSALALA.

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ameutaka Uongozi wa Shule ya Sekondari ya Mwl. Nyerere iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Msalala kutogeuza matumizi ya gari la kubebea wagonjwa (school ambulance) kuwa Daladal a, kuikodisha au kuifanya kuwa ya biashara kwa namna yoyote ile kwani kufanya hivyo ni kinyume na lengo kusudiwa.

RC Macha ameyasema haya Machi 3, 2025 akiwa kwenye hafla ya kukabidhi gari hilo ambapo pamoja na yote amewapongeza Wazazi, Bodi ya Shule pamoja na Wadau wa Elimu kwa kushiriki katika uchangiaji wa ununuzi wa gari hilo lililogharimu zaidi ya Tzs. Milioni 26.

“Ninawasihi sana uongozi wa shule hii, walimu na wote mnaohusika kutokengeuka na kugeuza matumizi ya gari hili ambalo nimelikabidhi leo kwa kuanza kuikodisha au kuifanya kuwa daladala badala yake ikafanye kazi kulingana na malengo yaliyokusudiwa kwa ambayo ni ya kubebea wanafunzi wanaokaa bweni ambao watapata changamoto kwa namna moja au nyingine za kiafya," alisema RC Macha.

Awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni ameupongeza uongozi wa shule, walimu na wadau wa elimu kwa jitihada za kuunga mkono Serikali katika kuboresha sekta ya elimu, lakini pia amewapongeza wanafunzi kwa matokeo mazuri kwa miaka 3 mfululizo.

Aidha Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mwalimu Nyerere Mwl. Kafuru Songora ameahidi kulitunza na kulisimamia gari hilo ili litumike kwa malengo yaliyokusudiwa ili lidumu kwa muda mrefu na kuwasaidia wanafunzi wanaokumbwa na changamoto za kiafya hususani kidato cha tano na sita ambao wanakaa bwenini.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe. Idd Kassim alisema kuwa, atashirikiana na uongozi wa Kata, Shule na wananchi katika kutatua changamoto kadhaa ambazo zililipotiwa kwenye hotuba iliyowasilishwa na kusisitizwa na baadhi ya wanafunzi ikiwemo ya upungufu wa madawati na matundu ya vyoo.

Pia Mhe. Idd aliahidi kutoa tofali 1000 kwa ajili ya kujenga Chumba Maalum cha watoto wa kike na Mashine ya kuvuta maji (motor) ambayo itakayokuwa ikitumika kuvuta maji katika kisima.

Picha ikionesha gari la wanafunzi

Picha ikionesha baadhi ya wanafunzi Sekondari ya Nyerere



Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • ENDELEENI KUTOA ELIMU ZAIDI KUHUSU AFYA YA AKILI - DC. MBONI

    May 30, 2025
  • TAKUKURU SHINYANGA YAANZA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA UBADHIRIFU WA SHILINGI MILIONI 92 ZA WAKULIMA WA TUMBAKU WA USHETU - DONASIAN.

    May 27, 2025
  • MAISHA BAADA YA KUSTAAFU YANAHITAJI UTULIVU - DC. MTATIRO

    May 26, 2025
  • MAFUNZO YA IPOSA NI MKOMBOZI KWA VIJANA WALIO WENGI WANAOKOSA FURSA YA ELIMU YA KAWAIDA - RC. MACHA

    May 23, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa