Na. Paul Kasembo, SHY RS
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ameipongeza Menejimenti, watumishi na wanafunzi wote wa Shule ya Savannah Plains High School kwa kupata ushindi wa Kimataifa na kutunukiwa Tuzo, Medali na Vikombe huku akisisitiza kuwa ushindi huu umeitangaza zaidi si tu Shule bali Mkoa wa Shinyanga katika nyanja za Kimataifa huku akitoa wito kwa shule nyingine zote mkoani Shinyanga kurejesha utaratibu wa Mijadala Mashuleni ili kuwajengea uwezo zaidi wanafunzi.
Hayo yamesemwa wakati wa mazungumzo kati yake na Uongozi wa Shule ya Savannah walipomtembelea ofisini kwake kwa lengo la kumjulisha juu ya uwepo wa mashindano na ushindi huu uliofanyika Jijini Nairobi Nchini Kenya ambapo Mataifa mbalimbali.
Katika Mashindano hayo yaliyofanyika jijini Nairobi nchini Kenya kuanzia Mei 9,2024 hadi Mei 12,2024 yakishirikisha nchi mbalimbali, Shule ya Sekondari Savannah Plains imepata ushindi wa Taasisi ya pili bora (The second best Institution), Washindi wa robo fainali (Quarter finalists), mzungumzaji bora wa Mdahalo kutoka Tanzania (The best debater from Tanzania) Hawarose Hassan Uledi, Mzungumzaji bora wa Nane (The eight best speaker)Allan Raymond Kabaya na imepata medali na tuzo ya washiriki bora wa mashindano.
Shule ya Sekondari Savannah Plains iliyopo Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga Mkoa wa Shinyanga nchini Tanzania imeendelea kufanya vizuri kwenye Mashindano ya Mjadala na Kuongea kwenye hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza na safari hii tena imerudi na ushindi na kutunukiwa tuzo, kombe na medali kwenye Mashindano ya Ubingwa wa Dunia wa Mijadala na Kuongea kwenye hadhara Afrika Mashariki ‘The East African World debate Championship’.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa