HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SHINYANGA YAANZA UPIMAJI WA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA BURE.
Na. Shinyanga RS.
HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa Shinyanga imeanza kutoa huduma ya Upimaji wa Magonjwa yasiyoambukiza (Presha, Moyo, Kisukari na Figo) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Magonjwa yasiyoambukiza Duniani.
Upimaji wa Magonjwa hayo umeanza rasmi jana Novemba 14, 2023 Hospitalini Mwawaza, ambao utachukua jumla ya siku tano (5) kuanzia leo jumatatu.
Mbali na upimaji huo, pia hospitali inafanya utoaji wa elimu ya afya pamoja na ushauri wa kitaalamu kuhusiana na magonjwa hayo unafanyika kwa kila anayefika kupima afua yake.
Zoezi la upimaji huanza saa 2:30 asubuhi hadi saa 9:30 alasiri na kilele itakuwa Ijumaa ya Novemba 17, 2023.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa