Na. Paul Kasembo, Shy Rs,
Kaimu Kamanda wa Polisi ACP Kennedy Mgani amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani limefanikiwa kukamata jumla ya makosa 5,048 ambayo makosa 3,460 yanahusisha magari, makosa 1,588 yanahusu bajaji na pikipiki huku wahusika wakiadhibishwa kwa kulipa faini za papo kwa hapo.
Aidha kwa upande wa utoaji wa elimu Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kufanya mikutano takribani 41 inayohusisha uelimishaji kwa jamii kuhusu usalama barabarani kupitia Shule, mikutano ya hadhara na vikundi 34 vya ulinzi shirikishi ili kuwawezesha kuzingatia Sheria za Usalama barabarani na kupunguza makosa ambayo yanaweza kugharimu uhai wao na wa wengine.
“Jeshi la Polisi linafanya jitihada nyingi kadiri iwezekanavyo kudhibiti na kupunguza makosa ya barabarani ambapo mpaka sasa tumekamata makosa takribani 5,048 yakihusisha makosa ya magari, pamoja na bajaji na pikiki huku wahusika wakipatiwa adhabu wanazostahili” amesema ACP Mgani.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linaendelea kuimarisha ulinzi na usalama kwa kushirikiana na Jamii pamoja na vyombo vingine vya ulinzi katika kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu kwa kufanya doria, misako, operesheni na kutoa elimu kwa wananchi.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa