Na. Paul Kasembo - MSALALA.
ALIYESEMEKANA kupatiwa Kadi ya Mpiga Kura iliyokuwa ikisomeka amezaliwa mwaka 1900 Bi. Sarah S. Lusobangeja mkazi wa kitongoji cha Mwabasabi, kijiji cha Kakola Namba 9 Kata ya Bulyanhulu amesema kuwa Kadi yake ya Mpiga Kura inasomeka amezaliwa tarehe 08/06/1988 na siyo 1900 kama ambavyo ilisekana awali.
Bi. Sarah ameyasema haya leo tarehw 25 Agosti, 2024 alipokuwa akizungumza na ujumbe wa wasimamizi wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Mpiga Kura uliongozwa na ndg. Bakari Kasinyo ambaye ni Mratibu wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Mkoa wa Shinyanga huku akisisitiza kuwa marekebisho ya Kadi hiyo yalifanyika tarehe ileile ya 22/8/2024 mara baada ya kuwa imebainika kuwa na makosa ya kiuandishi.
"Kadi yangu ya Mpiga Kura inasomeka vema nimezaliwa tarehe 08/06/1988 na siyo mwaka 1900 kama ambavyo imekuwa ikisemekana na walio wengi," amesema Bi. Sarah.
Akizungumza baada kufika katika kituo alichohudumiwa Sarah, Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Msalala ndg. Vicent Ipagala amesema kuwa marekebisho ya Kadi hiyo yalifanyika tarehe ileile ya 22/8/2024 mara baada ya kubaini uwepo wa tatizo la kiuandishi na hivyo akapatiwa Kadi nyingine yenye taarifa sahihi kama ambavyo inasomeka Kadi yake kwa sasa.
Haya yanafuatia baada ya uwepo wa kipande kifupi cha picha jongefu (video clip) kikionesha Kadi yake ya Mpiga Kura amezaliwa mwaka 1900 jambo ambalo lilipelekea hali ya sintofahamu miongoni mwa wananchi wanaomfahamu.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa