• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA AFYA NA MASUALA YA UKIMWI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MAAGIZO

Posted on: March 17th, 2025

Na. Paul Kasembo, Bulyanhulu - Kakola.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya Ukimwi Mhe. Hassan Mtenga akiwa ameongozana na wajumbe wake ameupongeza uongozi wa Mgodi wa Bulyanhulu kwa utekelezaji wa mpango wa Mgodi wa Bulyanhulu katika kudhibiti maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na kuajiri Watanzania zaidi ya asilimia 97.

Mhe. Mtenga ameyasema hayo leo Machi 16, 2025 baada ya Kamati hiyo kuutembelea na kuukqgua mradi wa Uchimbaji Madini wa Mgodi wa Bulyanhulu uliopo Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine Kamati hiyo imeridhishwa na na mpango wa mgodi huo unavyodhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

"Sisi kama Kamati tumeridhishwa na namna mgodi unavyoendesha kazi zake maana uwepo wa mradi huu kwa njia ya uwekezaji ni sifa kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwakuwa ndiye mlezi mkuu wa mradi huu, sisi kama Kamati tumefarijika kusikia kwamba 97% ni Watanzania wameajiriwa na wanafanya kazi kwenye mgodi huu na tunatoka hapa tukiwa na imani kubwa na mradi huu" alisema Mhe. Mtenga.

Meneja wa Mgodi wa Bulyanhulu ndg. Victor Lule amesema mgodi huo pamoja na uzalishaji wake bado umeendelea kuweka kipaumbele cha afya kwa watumishi wa mgodi huo ambapo huduma za afya kama zahanati, Huduma za kwanza hupatikana kwenye Mgodi huo na kwamba mgodi umekuwa ukipambana kuhakikisha watumishi wake wanaepukana na vitendo vitakavyopelekea kupatikana kwa waathirika wa magonjwa ya kuambukiza ikiwemo VVU jambo ambalo linashughuliliwa na Kamati hiyo.

Katika hatua nyingine Naibu waziri wa Madini Dkt Steven Kiruswa kwa niaba ya Serikali amesema maelekezo yaliyotolewa na Kamati hiyo yatafanyiwa kazi kwa lengo la kuboreshaji uzalishaji kwenye mradi wa  mgodi wa Bulyanhulu ambapo Serikali ndio mbia mkuu katika mradi huo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amesema uwepo wa Mgodi wa Bulyanhulu unayo manufaa makubwa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala na hata Mkoa wa Shinyanga kwa ujumla, hivyo kitendo cha Kamati ya Afya na Maswala ya Ukimwi kutembelea mgodi huo kitarahisisha malengo yaliyowekwa na mgodi  yanafikiwa ipasavyo.

Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • ENDELEENI KUTOA ELIMU ZAIDI KUHUSU AFYA YA AKILI - DC. MBONI

    May 30, 2025
  • TAKUKURU SHINYANGA YAANZA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA UBADHIRIFU WA SHILINGI MILIONI 92 ZA WAKULIMA WA TUMBAKU WA USHETU - DONASIAN.

    May 27, 2025
  • MAISHA BAADA YA KUSTAAFU YANAHITAJI UTULIVU - DC. MTATIRO

    May 26, 2025
  • MAFUNZO YA IPOSA NI MKOMBOZI KWA VIJANA WALIO WENGI WANAOKOSA FURSA YA ELIMU YA KAWAIDA - RC. MACHA

    May 23, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa