Na. Shinyanga RS
KAMATI ya Siasa Mkoa wa Shinyanga imehitimisha ziara yake ya utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020/2025 katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ambapo pamoja na pongezi kwa utekelezaji mzuri wa Ilani lakini pia Kamati imeishauri Serikali kuboeresha na kuimarisha kivuko cha wananchi kuingia soko jipya la Ibinzamata.
Hayo yamebainishwa tarehe 24 Februari, 2024 na Ndugu John Siagi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga ambaye alimuwakilisha Mwenyekiti CCM Mkoa wa Shinyanga Ndugu Mabala Mlolwa ambaye alipata udhuru huku akisisitiza pia uboreshwaji wa mazingira katika Shule mpya ya Sekondari Butengwa ambapo amewataka kupanda miti ya matunda na vivuli.
Awali Kamati ilikagua utekelezaji wa Ilani katika Shule mpya ya Wasichana Shinyanga ambapo ameitaka Serikali kusimamia vema ujenzi wa majengo ili yawanufaishe na vizazi vijavyo, huku akipongeza zaidi ujenzi wa jengo la wagonjwa wa dharula Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga ambapo pia alisisitiza kuzingatiwa kwa uadilifu, maadili ya kazi zao na utendaji kazi bora ukizingatia kuwa wanahudumia wananchi.
"Tuipongeze Serikali kwa utekelezaji wa Ilani yetu ya CCM 2022/2025 katika sekta ambazo Kamati imekagua, na kwamba maelekezo na ushauri uliotolewa na Kamati uzingatiwe na utekelezwe haraka zikiwemo kasoro zote zilizobainika ili wananchi wanufaike na utekelezaji huu wa Ilani", amesema Ndugu Siagi.
Kwa upande wa Serikali, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ambaye hakuwepo baada ya kupata udhuru alisema kuwa, Serikali imepokea kwa unyenyekevu na uzito wa aina yake maelekezo yote yaliyotolewa na Kamati ya Siasa Mkoa na kwamba ndani ya muda mfupi Serikali itakuwa imetekeleza kikamilivu.
Aidha, Prof. Siza Tumbo ambaye ni Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya RC MNDEME aliongezea kwa kusema kuwa, utekelezaji wa maelekezo ya Kamati utafanyika kwa harhaka sana na kwa weledi mkubwa ili wananchi wanufaike na huduma zitolewazo na Serikali
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa