Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack ametoa wito kwa wananchi kuwa na tabia ya kufanya mazoezi ya viungo kila mara ili kujiepusha na magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanayosababishwa na mfumo mbaya wa maisha ikiwemo kutofanya mazoezi.
Mhe. Telack ametoa wito huo alipofungua rasmi kampeni ya kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza kwa njia ya mazoezi iliyofanyika katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Shinyanga (Shycom) hivi karibuni.
Kampeni hiyo ya Kitaifa iliyofanyika kufuatia agizo la Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu la kutenga siku ya mazoezi kwa wananchi wote, imefanyika na kuungwa mkono na wananchi waliojitokeza kwa wingi kufanya mazoezi hayo.
Aidha, Mhe, Telack amesema kampeni hiyo ni endelevu na kwamba kila Jumamosi ya pili ya Mwezi mazoezi ya viungo yatafanyika kwa pamoja kwa wananchi wote, hata hivyo amewahimiza kuendelea kufanya mazoezi majumbani na sehemu maalumu zilizotengwa ili kuimarisha afya zao.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa