MGANGA Mkuu Mkoa wa Shinyanga Daktari Yudas Ndugile amewataka Maafisa Afya wa Halmshauri za Mkoa wa Shinyanga kwenda kutekeleza Miradi ya Uendelevu wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (e- WASH) kwa kuzingatia kanuni na taratibu ili miradi hiyo imalizike kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa uliokusudiwa.
Ameyasema haya leo Februari 4, 2025 wakati akifungua Mafunzo ya Mfumo wa Kielekroniki wa Manunuzi ya Umma (NeST) katika Miradi ya Uendelevu wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (e- WASH) unaotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Msalala, Shinyanga na Ushetu kwenye ujenzi wa miundombinu ya maji na usafi wa mazingira.
“Ninawaasa mkazingatie kanuni na taratibu mnapoenda kutekeleza miradi ya uendelevu wa maji na usafi wa mazingira kwenye Halmashauri zenu kwani mafunzo haya yatawasaidia kwa kiasi kikubwa kutekeleza miradi hii kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa,” amesema Dkt. Yudas.
Aidha amewakumbusha maafisa afya kuzingatia mahitaji ya msingi ya kituo kabla ya kuanza ujenzi wa mifumo ya kuhifadhi vyanzo vya maji katika vituo vya afya ili kuepuka matumizi makubwa yasiyo ya lazima.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa