Na. Paul Kasembo, SHY RS.
KATIBU Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni leo tarehe 26 Agosti, 2024 amefika kwenye Kituo cha Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura kilichopo Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Lubaga hapa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na kuboresha taarifa zake.
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura kwa Mkoa wa Shinyanga lililoanza tarehe 21 Agosti, 2024 litakamilika tarehe 27 Agosti, 2024 ambapo litakuwa limeendeshwa kwa siku saba huku wito na hamasa ukiendelea kutolewa zaidi kwa wananchi kutumia vema muda huu uliobakia kuweza kupata huduma hii katika vituo mbalimbali ambavyo huanza kufunguliwa saa 2:00 asubuhi na hufungwa ifikapo saa 12:00 jioni.

OFISI YA MKUU WA MKOA, MKOA WA SHINYANGA, 04 MTAA WA BOMA
Anuani: P.O.Box 320, 37180,SHINYANGA, TANZANIA
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa