Na. Paul Kasembo, SHY RS.
KATIBU Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni amekutana na Timu ya Wataalam ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambayo imejitambulisha kwake, huku RAS CP. Hamduni akisisitiza uwajibikaji, uzalendo, uadilifu na misingi ya sheria kufuatwa na hili ni kwa watumishi wote Mkoa wa Shinyanga.
Haya yamesemwa leo tarehe 22 Agosti, 2024 ofisini kwake ikiwa ni siku ya kwanza kuripoti mkoani Shinyanga ikiwa ni kituo kipya cha kazi baada ya kuteuliwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga baada ya aliyekuwepo kurejeshwa Chuo cha Kilimo Sokoine ambako alikuwa Mkufunzi Mwandamizi.
"Pamoja na kuwaomba ushirikiano, lakini pia niwatake kila mmoja atekeleze wajibu na majukumu yake kikamilifu kwa kutanguliza uzalendo, uadilifu, nidhamu na kufuata misingi ya sheria," amesema CP. Hamduni.
Akitoa salumu kwa niaba ya Menejimenti na watumishi Mwl. Dafroza Ndalichako amesema kuwa watumishi wataendelea kumkumbuka sana Prof. Siza Tumbo kwa utendaji kazi wake mzuri ambao alikuwa Mwalimu wakati wote ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.
Kwa upande wa CP. Hamduni, Mwl. Ndalichako amemkaribisha kwa mikono miwili huku akimuahidi ushirikiano wakati wote ili aweze kutimiza adhima ya utekelezaji wa majukumu yake hapa mkoani Shinyanga, na kwamba watumishi wote wapo tayari kupokea maelekezo, ushauri na maoni wakati wote atakapoelekeza.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa