Na Paul Kasembo, SHY DC,
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amesema kuwa, Kijiji cha Sayu kilichopo Kata ya Pandagichiza Wilaya ya Shinyanga ndiyo kinara wa uzalishaji wa zao la pamba Mkoa wa Shinyanga kwani kina wakulima ambao wamelima pamba na kupata kwa wingi zaidi tofauti na maeneo mengine.
RC Macha ameyasema hayo leo Februari 19, 2025 wakati akihitimisha ziara ya kukagua na kuhamasisha kilimo cha pamba mkoani Shinyanga ambapo alitembelea Halmashauri ya Wklaya ya Ushetu, Kishapu na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambapo huku akisisitiza kuwa katika maeneo yote aliyotembelea lakini Kijiji cha Sayu ndiyo kimeibuka kinara katika uzalishajin wa pamba kulinganisha na maeneo mengine.
“Niwapongeze sana ninyi wakulima wa pamba katika Kijiji hiki ya Sayu na kuwa kinara wa uzalishaji wa zao la pamba hapa Shinyanga, nimepita na kutembelea wakulima wengi lakini ninyi mmekuwa mfano bora wa kuzalisha kilo nyingi kwa hekari moja ambapo hapa kuna mwenye kilo 2200 kwa hekari, kilo 1800, kilo 1600 na wa chini kabisa alipata kilo 1340 kwa hekari 1, huu ni mfano bora sana na wakuigwa” amesema RC Macha.
RC Macha ameongeza kuwa Serikali ina malengo ya kuhakikisha wakulima wanafurahia kilimo cha pamba na kuvuna kuanzia kilo 1200 na kuendelea kwa hekari moja katika maeneo yote mkoani Shinyanga ingawa Wilaya ya Shinyanga inaonesha wakulima wengi wamekuwa wakinufaika na kupata faida kubwa tofauti na maeneo mengine kwani kwa hekari moja wanapata zaidi ya kilo 1000.
Aidha RC Macha amempongeza na kumtolea mfano ndugu Andrea Maganga mkulima wa pamba kutoka Kijiji cha Sayu, Kata ya Pandagichiza aliyeibuka mshindi wa pili wa kilimo cha pamba nchini na kupewa zawadi ya Tzs. Milioni 5 ambaye hulima kwa kuzingatia kipimo cha Sentimita 60x30 kwani kina tija zaidi na mkulima anaweza akapata kilo takribani 2200 kwa hekari 1.
Awali akizungumza na wakulima, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Julius Mtatiro (Wakili) alimtaka Afisa Ugani Kilimo kupima ukubwa wa mashamba ya pamba ili ifahamike kitaalam ukubwa wake na uwekwe kwenye kumbukumbu sahihi za ofisi na kwa matumizi ya rejea pia.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa