Mratibu wa Utawala kutoka Ofisi ya Rais Bw. Francis Manyira amewataka watumishi nchini kuhakikisha mwananchi yeyote anayehitaji huduma katika Ofisi za Umma, anapata ufumbuzi kwa kumuelekeza sehemu sahihi ya kupata huduma anayohitaji au kumshughulikia kama shida hiyo ipo kwenye eneo lake.
Akizungumza na watumishi wa Umma wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Taasisi za Umma, mapema leo tarehe 08/04/2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Bw. Manyira amesema ni wajibu wa kila Mtumishi wa Umma katika nafasi yake kuwatumikia wananchi kwa sababu watumishi ni sehemu ndogo ya jamii wenye dhamana ya kutoa huduma kwa Umma kulingana na taratibu na mifumo iliyowekwa.
Amewasisiza watumishi kutumia kauli nzuri na unyenyekevu na kuwajali wananchi na wateja wanaofika kwenye ofisi zao.
Naye Mratibu Msaidizi wa Utawala wa Ofisi ya Rais Bi Hilda Lugembe amewasisitiza Watumishi wote kufuata Sheria, Taratibu na Kanuni zilizowekwa katika kutekeleza majukumu yao.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa