Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamiringi Macha amewataka wagombea wanaotarajia kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga kuwa na shughuli halali zinazowapatia uchumi na kuendesha maisha yao badala ya kutegemea kuja kunufaika watakapoingia madarakani.
RC Macha ameyasema haya leo tarehe 8 Oktoba, 2024 wakati akizindua zoezi la uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura kwa ajiri ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika viwanja vya Sabasaba Kambarage Manispaa ya Shinyanga hafla ambayo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Julius Mtatiro, Mstahiki Meya Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko, ndg. Bakari Kasinyo aliyemuwakilisha RAS Shinyanga, Waheshimiwa Madiwani na umati mkubwa wa wananchi.
“Nitoe rai kwa wagombea wote ambao wanatarajia kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba, 2024 kuhakikisha mnakuwa na shughuli halali za kiuchumi ambazo zinawasaidia kuendesha maisha yenu badala ya kuja kutegemea kipato cha pesa katika nafasi hizi ili muendeshe maisha yenu hiyo hapana” amesema RC Macha
Akizungumza katika viunga hivi vya hafla, Mstahiki Meya Mhe.mElias Masumbuko amewaomba wananchi wenye sifa za kupiga kura kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandisha kwenye Daftari la Wapiga Kura katika Serikali za Mitaa ili waweze kuchagua viongozi bora watakaotimiza malengo yao kwa miaka mitano ijayo.
Zoezi la Uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura linatarajiwa kuanza tarehe 11-20 Oktoba 2024 huku Uchaguzi huu unatarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024 ambapo utafanyika katika mitaa 90, vijiji 506, pamoja na vitongiji 2704 katika Mkoa wa Shinyanga.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa