Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amempa siku 2 mmiliki wa kiwanda cha nyama kilichopo katika Manispaa ya Shinyanga kuondoka mara moja na kukabidhi kiwanda hicho kwa Serikali baada ya kushindwa kukiendesha na kubainika kukiuza kinyemela kwa Kampuni ya Agro ranch ya Mkoani Kagera.
Mhe. Telack ametoa agizo hilo alipotembelea kiwanda hicho akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na kumkuta msimamizi wa kampuni ya Agro ranch aliyejitambulisha kwa jina la Samwel Kombe aliyebainisha uuzwaji wa kiwanda hicho.
Mhe. Telack amesema kuwa, kuanzia sasa kiwanda hicho kitakuwa chini ya Serikali na kwamba mali zote zilizokabidhiwa kwa Triple S zirudishwe mara moja .
Kiwanda hicho kilichojengwa na Serikali tangu mwaka 1975 kiliuzwa kwa Triple S miaka 10 iliyopita na hadi sasa hakuna uzalishaji uliofanyika.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa