Na. Paul Kasembo, SHINYANGA DC.
KATIKA kuelekea Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoani Shinyanga, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imeanza rasmi mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendesha vifaa vya Bayometriki katika ngazi ya Kata huku wito ukitolewa kwa wananchi wote kujitokeza kuanzia siku ya Jumatano tarehe 21 hadi 27 Agosti, 2024 zoezi ambalo litadumu kwa muda wa siku saba kila kituo.
Akizungumza mara baada ya kushuhudia kiapo cha kutunza Siri kwa Waandishi Wasaidizi na Waendesha vifaa vya Bayometriki Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Mratibu wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoa wa Shinyanga Bw. Bakari Kasinyo amesema kuwa uboreshaji utafanyika katika vituo vilivyopo kwenye Mitaa, vijiji na vitongoji ambapo muda wa kufungua vituo utakuwa ni saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa