• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

KULWA LENIS ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA WA SHIRECU

Posted on: March 28th, 2024

Na. Paul Kasembo - SHINYANGA RS.

MKUTANO Mkuu wa 29 wa Chama cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga [SHIRECU (1984) LTD] umemchagu Ndugu Kulwa Lenis Jishanga kuwa Mwenyekiti wake mpya baada ya uchaguzi uliowahusisha wajumbe wa SHIRECU tarehe 26 Machi, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano uliopo katika jengo la SHIRECU hapa Manispaa ya Shinyanga, huku Ndungu Jishanga akiwataka wanaSHIRECU kuwa wamoja na waitumikie Ushirika kwa moyo mmoja, uzalendo na kujituma ili waweze kuirejeshea hadhi yake ya zamani.


Uchaguzi huu uliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa zamani Ndg. Josephati Limbe, umejumuisha wajumbe wote huku Limbe akisema kuwa huu ni utekelezaji wa kawaida wa matakwa ya Ushirika ili kuweza kutekeleza mipango na mikakati iliyojiwekea kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ambayo ni pamoja na ununuzi wa Kiwanda kipya cha kuchambua Pamba, ununuzi wa Pamba Mbegu, ujenzi wa Ghala la kisasa katika Kanda ya Solwa na Ukumbi wa kisasa wa Mikutano utaokuwa na uwezo wa kuchukua watu elfu 5.


"Ndugu wajumbe, pamoja na mamno mengine, lakini pia Ushirika unaleta kwenu mipango mkakati kadhaa ili muweze kuridhia itekelezwe ikiwemo ununi wa Kiwanda kipya cha kuchambua Pamba na unnuzi wa Pamba Mbegu kwa msimu wa mwaka 2024/2025, na hii i akwenda sambamba na ombi la Bodi kwenu ili mridhie ukopaji wa fedha zaidi ya Bil. 5 kutoka Benki ya TADB ili kuweza kutekeleza miradi hii ya kimkakati," amesema Limbe.


Awali Mhe. Julius Mtatiro ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga aliyemuwakilisha RC Shinyanga Mhe. Anamringi Macha alisema kuwa, wanaushirika wamepata bahati sasa kwakuwa wamepata DC ambaye ni mwanaushirika pia, hivyo atahakikisha kuwa Vyama vya Ushirika na wakulima wanakuwa na tija katika pamoja na kuirejesha SHIRECU katika hadhi yake kama zamani.


Aidha Kaimu Meneja SHIRECU Bi. Asnath Changamike alisoma taarifa huku akiwaomba wajumbe kuridhia mapendekezo ya makisio ya bajeti kwa mwaka 2024/2025 yenye zaidi ya Bil. 1.4 ambapo wajumbe walipitisha pia bajeti hii.


Mkutano umewapatia dhamana Ndg. Kulwa Jishanga kuwa Mwenyekiti, Bi. Naomi Masega - Makamu M/kiti, na wajumbe ni Mussa Robert, Dasse Dotto, Fransic Daniel na Philipo Lunegula.


MATUKIO KATIKA PICHA


Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga akifungua mkutano wa wadau


Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akielezea jambo kabla ya uchaguzi


Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • ENDELEENI KUTOA ELIMU ZAIDI KUHUSU AFYA YA AKILI - DC. MBONI

    May 30, 2025
  • TAKUKURU SHINYANGA YAANZA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA UBADHIRIFU WA SHILINGI MILIONI 92 ZA WAKULIMA WA TUMBAKU WA USHETU - DONASIAN.

    May 27, 2025
  • MAISHA BAADA YA KUSTAAFU YANAHITAJI UTULIVU - DC. MTATIRO

    May 26, 2025
  • MAFUNZO YA IPOSA NI MKOMBOZI KWA VIJANA WALIO WENGI WANAOKOSA FURSA YA ELIMU YA KAWAIDA - RC. MACHA

    May 23, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa