Na. Paul Kasembo, SHY RS.
m-mama ni mfumo wa Rufaa na Usafiri wa dharura kwa mama mjamzito, aliyejifungua na mtoto wa mchanga ambapo leo Wanahabari kutoka Mikoa ya Shinyanga, Tabora, Kigoma na Simiyu ambao wanahudumu katika Redio za Kijamii wameshiriki mafunzo haya ambapo pamoja na mambo mengine watapata kujuwa kwa usahihi matumizi ya kupiga namba 115 ya dharura kutoka kwa mgonjwa au ndugu kwenda Kituo cha Afya kichokaribu naye na ili ambayo hupigwa na mhudumu wa afya aweza kuwa Nesi au Daktari kwenda Kituo kingine cha afya.
Aidha, mada mbalimbali zitawasilishwa ikiwemo Mbinu jumuishi za ushirikishwaji wa jamii kuhusu mfumo wa m-mama iliyowasilishwa na Flora Kajumulla ambaye ni Mratibu wa m-mama na Afisa Muuguzi Mkuu kutoka Mkoa wa Shinyanga, wajibu na majukumu ya Maafisa Habari wa Mikoa na Wanahabari katika kuhabarisha umma.
Huduma hii ni bure kabisa na hakuna malipo. m-mama, Okoa Maisha piga simu 115 BURE.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa