• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

MAAFISA TARAFA NA WATENDAJI KATA MKOA WA SHINYANGA WAPEWA MAFUNZO, WAHIMIZWA KUIMARISHA UKUSANYAJI MAPATO NA UADILIFU

Posted on: November 30th, 2023

Na. Shinyanga RS.

Maafisa tarafa na watendaji wa kata Mkoani Shinyanga wametakiwa kuimarisha uadilifu na kusimamia kikamilifu suala zima la amani na ushirikiano baina yao na wananchi sambamba na kusimamia ukusanyaji wa mapato ndani ya mamlaka ya serikali za mitaa.

Hayo yamesemwa leo Novemba 30, 2023 na Afisa elimu Mkoa wa Shinyanga Dafroza Ndalichako wakati akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa tarafa na watendaji wa kata waliopo ndani ya mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika kwa muda wa siku mbili kwenye ukumbi wa mikutano katika Chuo cha Ualimu Shinyanga (Shycom).

Ndalichako amewasihi viongozi hao wa ngazi ya tarafa na kata kuyaishi yale waliofundishwa lakini pia kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato ya serikali kwa kutumia mifumo iliyowekwa.

“Wote ni mashahidi kuwa sehemu yoyoye ambayo haina amani na utulivu wananchi hawataweza kushiriki shughuli za maendeleo na hivyo kuathiri ukuaji wa uchumi, hivyo nendeni mkaimarishe amani, utulivu na mshikamano lakini pia kasimamieni ukusanyaji wa mapato. Usimamizi wa mapato ndani ya mamlaka ya serikali za mitaa utaendelea kuwa kipaumbele cha serikali sambamba na matumizi ya mifumo ya kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato", amesema Ndalichako.

Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeleta fedha nyingi katika mamlaka ya serikali za mitaa kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali hivyo ni wajibu wenu kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ndani ya maeneo yenu, mkasimamie na kufuatilia fedha za miradi zinazotolewa na serikali ili ikawe na tija kwa wananchi na kuondoa changamoto ya kukosa huduma.

"Makusudio ya kutoa mafunzo haya kwenu kupitia ofisi ya Rais TAMISEMI  ni kwa sababu serikali inatarajia mabadiliko makubwa ya utendaji kazi wenu katika kuwahudumia wananchi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu ili kuharakisha maendeleo katika sekta mbalimbali, kupitia mafunzo haya nendeni mkatekeleze majukumu yenu kwa ubora zaidi, ni matarajio yetu Shinyanga itakuwa ni sehemu ya mfano”, ameongeza Ndalichako.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa serikali za mitaa kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Hamisi Mkunga amewataka wakawe walimu kwa wengine ambao hawakupata nafasi ya kushiriki mafunzo yaliyohusu  maadili na majukumu kama viongozi wa ngazi husika

“Leo tunahitimisha Mafunzo haya ya awamu ya pili ya kuwajengea uwezo maafisa tarafa na watendaji kata yaliyohusisha mikoa nane ambayo ni Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Pwani, Dae es salaam, Lindi na Mtwara, kile tulichokipata kupitia mafunzo haya tukawe walimu kwa watu wengine ambao hawakupata nafasi ya kushiriki mafunzo haya lakini pia mafunzo haya yawe chachu ya mabadiliko kwenye majukumu yetu ya kila siku na pia ofisi ya taifa TAMISEMI itahakikisha unawapima kwa kile kilichoelekezwa”, amesema Mkunga.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Abel Kaholwe na Emmanuel Enock wameishukuru ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kutoa mafunzo hayo kwani itaenda kuongeza chachu ya utendaji kazi kwenye maeneo mbalimbali.

“Kwanza tunamshukuru Mheshimiwa Rais kupitia ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kutuletea mafunzo haya yatakayokwenda kuongeza chachu ya utendaji kazi kwenye maeneo yetu na kutukumbusha wajibu wetu kama viongozi pamoja na kuzingatia kanuni na maadili ya kazi yetu”, amesema Emmanuel Enock.


HABARI PICHA


Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Dafroza Ndalichako akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo.


Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Hamisi Mkunga akizungumza wakati wa mafunzo hayo.

Mkuu wa Idara ya Mafunzo ya muda mfupi TPSC Hosea Goerge akitoa mafunzo.



Afisa Mtendaji Kata ya Mwamasa Halmashauri ya Msalala Abel Kaholwe akizungumza mara baada ya mafunzo hayo.


Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • ENDELEENI KUTOA ELIMU ZAIDI KUHUSU AFYA YA AKILI - DC. MBONI

    May 30, 2025
  • TAKUKURU SHINYANGA YAANZA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA UBADHIRIFU WA SHILINGI MILIONI 92 ZA WAKULIMA WA TUMBAKU WA USHETU - DONASIAN.

    May 27, 2025
  • MAISHA BAADA YA KUSTAAFU YANAHITAJI UTULIVU - DC. MTATIRO

    May 26, 2025
  • MAFUNZO YA IPOSA NI MKOMBOZI KWA VIJANA WALIO WENGI WANAOKOSA FURSA YA ELIMU YA KAWAIDA - RC. MACHA

    May 23, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa