Na. Shinyanga RS
MAFUNZO ya mfumo mpya wa ununuzi NeST kwa wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga yamefungwa leo tarehe 14 Septemba, 2023 huku Afisa Elimu Watu Wazima Mkoa wa Shinyanga Ndg. Dedan Rutazika akiwataka walaalam wenzake kwenda kutanguliza uzalendo na kufuata seheria wakayi wote wa kuutumia mfuno huu
Rutazika ambaye amefunga mafunzo haya kwa niaba ya Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga amesema kuwaNeST ni mfumo rafiki sana kwa Wakuu wa Sehemu na Vitengo ambapo itawasaidia kuandaa mpango kazi wa manunuzi kulingana na hitajio la Ofisi husika.
"Mfumo huu mpya wa ununuzi NeST utakaoanza rasmi Oktoba 1, 2023 ni mfumo rafiki sana utakaokuja kuondoa kabisa uagizaji na ununuzi wa bodhaa feki, kuondoa mianya ya rushwa, urasimu hautakuwa na nafasi katika mfumo huu na utakaorahisisha utoaji na upatikanaji wa huduma tena kwa wakati," alisema Rutazika.
Mfumo huu wa NeST unakuja kuchukua nafasi ya mfumo wa TANePS ambao utafika ukomo wake rasmi ifikapo Septemba 30, 2023 na hivyo kutoa fursa kwa mfumo huu mpya wa NeST kuanza kutumika rasmi Octoba 1, 2023.
Picha ikimuonesha Dedan Rutazika akizungumza jambo wakati kufunga mafunzo ya NeST kwa wataalam
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa