• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

MAKABIDHIANO YA MRADI YAFANYIKA BUGARAMA, HALMASHAURI YA MSALALA - SHINYANGA

Posted on: May 24th, 2023

Na. Shinyanga RS

Hafla ya makabidhiano ya Mradi wa Kufikia Usawa wa Kijinsia kwa kuwawezesha Wanawake na Wasichana Balehe kwa kuwainua kiuchumi imefanyika leo tarehe 24 Mei, 2023 kati ya Serikali ya Mkoa wa Shinyanga na Wadau katika Kata ya Bugarama iliyopo Halmashauri ya Msalala Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi Mhe. Christina Solomon Mndeme aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita.

Katika makabidhiano hayo Mhe. Mboni aliwaeleza wananchi, wadau wa masuala ya kijinsia na wanafunzi waliokuwa wamehudhuria hafla hiyo kuwa Serikali inawashukuru sana wadau wote walioshiriki katika kutekeleza ujenzi wa mradi huo wakiwamo KOICA, UNFPA, UN WOMEN na watekelezaji wa mradi huo (KIWOHEDE, TAHA, TGNP, C-SEMA) kwa kushiriki kikamilifu tangu mwanzo hadi mwisho ambapo leo mradi unakabidhiwa.

“Leo hii tunakabidhiwa majengo mawili yaliyojengwa ambayo ni HUDUMA JUMUISHI (ONE STOP CENTER) na DAWATI LA JINSIA LA POLISI ambavyo hivi vinahusika katika kuhakikisha kuwa vinatoa huduma Rafiki na zinazojitoshereza, lengo ni kuhakikisha kuwa wahanga wa vitendo vya ukatili wanapatiwa huduma zinazostahiki kwa walengwa waweze kuedelea kuishi salama bila kuhisi unyonge wala udhaifu wakati wote,” alisema Mhe. Mboni.

Kando na hayo, Mhe. Mboni alitoa angalizo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Ndg. Charles Fussi na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kahama (OCD) kuhakikisha kuwa majengo haya hayabadilishi matumizi kwa namna yoyote ile huduma zilizokusudiwa kutolewa kwenye majengo haya zinasimamiwa kwa weledi mkubwa na utoe matoe makubwa zaidi ya haya.

Akitoa salamu kwa niaba ya Pro. Siza Tumbo ambaye ni Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga Ndg.Tedson Ngwale alisema kwamba kukamilika kwa mradi huo ni furaha kwa Serikali na kwamba mradi huo ndiyo utakuwa wa mfano katika kufikia Usawa wa Kijinsia na kuwawezesha wanawake na mabinti kiuchumi na kwamba mradi huo utakuwa ni endelevu huku akiwaahidi wadau hao ushirikiano Zaidi katika miradi mingine.

Katika hafla hiyo, mgeni rasmi aliweza kutembelea na kuona shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Kikundi cha Wanawake (LUMOLUMO WOMEN GROUP) kilichopo Kijiji cha Namba Moja Kata ya Segese Halmashauri ya Msalala ambacho kinaendesha shughuli za kilimo na kuweza kujipatia mafanikio makubwa ambapo mpaka sasa wanayo Akiba ya Milioni 5 Benki huku wakiomba Milioni 22 waweze kufungua duka kubwa ombi ambalo lilipokelewa na Mhe. Mboni na kuahidi kulishughulikia kupitia kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ambaye alisema watapewa kupitia mkopo wa asilimia 10.

Picha ya pamoja ikimuonesha Mhe. Mboni Mhita (aliyevaa suti nyeusi) na wadau mbalimbali wakati hafla hiyo

Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • WANUFAIKA WA MIKOPO YA 10% LIPENI KWA WAKATI ILI PIA VIKOPESHWE NA VIKUNDI VINGINE - RC MACHA

    February 13, 2025
  • CP. HAMDUNI AKUTANA NA KAMATI YA MICHEZO YA JWTZ

    February 13, 2025
  • WANANCHI, LIPENI KODI YA ARDHI KWA WAKATI MUEPUKE RIBA - LEO KOMBA

    February 12, 2025
  • WAJUMBE WA BODI, TUMIENI TAALUMA ZENU KUISAIDIA HOSPITALI KUKAMILISHA MIRADI YA UJENZI- RAS CP. HAMDUNI.

    February 11, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa