Repost @shinyangamanispaa
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imeibuka mshindi wa pili kitaifa katika mashindano ya afya na usafi wa mazingira kwa mwaka 2024, ikitangazwa miongoni mwa Halmashauri za Manispaa 20 nchini, ushindi huu umeambatana na tuzo ya heshima pamoja na zawadi ya shilingi milioni 2 (Tsh 2,000,000) iliyotolewa na Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama (MB).
Tuzo hiyo ilipokelewa kwa heshima kubwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Elias R. Masumbuko, akiwa pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Usafi wa Mazingira na Udhibiti wa Taka, Ndg. Kuchibanda Snatus, hafla hiyo muhimu ilifanyika tarehe 08 Aprili 2025, mkoani Dodoma.
Ushindi huu ni uthibitisho wa jitihada kubwa zinazofanywa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga katika kuhakikisha mazingira safi, salama na yenye afya kwa wakazi wake, sambamba na kutekeleza kwa vitendo mikakati ya kitaifa ya usafi wa mazingira.
Manispaa inaendelea kuwashukuru wananchi wote kwa ushirikiano wao wa dhati na inawaomba kuendeleza juhudi za usafi wa mazingira kwa ustawi wa jamii na vizazi vijavyo.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa