Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde ametoa siku 14 kwa Mkurugenzi wa Mgodi wa El – Hillary uliopo Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga, kujisajili katika mfuko wa fidia kwa watumishi (WCF) na kulipa faini kwa kuchelewesha malipo ya usajili.
Mhe. Mavunde ametoa agizo hilo mapema Jumanne hii alipofanya ziara ya kushtukiza mgodini hapo, akiambatana na Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko kwa lengo la kufuatilia hatua za utekelezaji wa agizo la Serikali lililowataka waajiri wote kujisajili katika mfuko wa fidia ifikapo tarehe 30 Septemba, 2017.
Amesema Serikali, pamoja na kulinda maslahi ya watumishi, pia ina nia njema ya kuwapunguzia waajiri jukumu la kuwahudumia watumishi walioumia kazini.
Mavunde amewataka waajiri kuwa na utamaduni wa kutii sheria zilizowekwa siyo hadi kusikia Waziri anakuja kufuatilia ndiyo wanalipa fidia hiyo.
Aidha, Mhe. Mavunde ameutaka uongozi wa mgodi huo kufuatilia maelekezo ya Ofisi ya Kazi Mkoa, kuhakikisha inawapatia watumishi wake zaidi ya 160 mikataba ya kazi inayokidhi matakwa ya kisheria.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa