Na. Paul Kasembo, SHY RS.
NAIBU Waziri wa Madini Mhe. Dr. Steven Kiruswa (Mb)leo tarehe 25 Julai, 2024 amemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ofisini kwake ambapo pamoja na mazungumzo mengine lakini pia Mhe. Kiruswa amempongeza sana RC Macha kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuhakikisha wananchi wake wanapata maendeleo na kumshukuru kwa mapokezi yake mazuri.
Aidha kwa upande wake RC Macha amemueleza Mhe. Kiruswa kuwa Mkoa wa Shinyanga unaendelea vema kabisa na utekelezaji wa shughuliza mbalimbali za kuwaletea maendeleo wananchi ikiwemo na uchimbaji wa madini na kuhakikisha kuwa maono ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yanatafsiriwa kwa vitendo katika vijiji vyote 506 kupitia Sekta mbalimbali mkoani Shinyanga.
HABARI PICHA
Mhe. Dr. Steven Kiruswa
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa