Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MAKAMU Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania (INEC), Mhe. Jaji (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk, ameridhishwa na utekelezaji wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani Shinyanga.
Mhe. Mbarouk alitembelea na kukagua baadhi ya Vituo hivyo ambavyo vimeanishwa na kutambulishwa katika Ofisi za Watendaji wa Kata huku akitoa pongezi kwa namna ambavyo kazi ya usimamizi, ufuatiliaji na utekelezaji wa zoezi hili unavyoendelea.
Pamoja na pongezi hizo, pia ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa wananchi wwnye sifa kuzitumia vyema siku saba (Mei 1 - 7, 2025) zilizotengwa kwa ajili ya uboreshaji, ili waweze kushiriki kikamilifu katika zoezi la kupiga na kupigiwa kura wakati utakapowadia.
OFISI YA MKUU WA MKOA, MKOA WA SHINYANGA, 04 MTAA WA BOMA
Anuani: P.O.Box 320, 37180,SHINYANGA, TANZANIA
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa