Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Anthony Mavunde amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini ambao bado hawajatekeleza agizo la Serikali la kutenga maeneo kwa ajili ya kuweka vitalu nyumba (green house) wafanye hivyo ili kuwasaidia vijana kupata sehemu za kujiajiri na kupunguza tatizo la ajira.
Mavunde ametoa agizo hilo mapema wiki hii alipofanya ziara ya siku mbili kwa lengo la kukagua utengaji wa maeneo hayo Mkoani Shinyanga ambapo amesema Mkoa wa Shinyanga ni moja ya Mikoa saba ya kwanza kunufaika na mradi wa kitalu nyumba kupitia mfuko wa maendeleo ya vijana unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Amewataka Wakurugenzi kutumia mfuko wa maendeleo ya vijana, kukopa fedha ili kuwawezesha vijana kuendesha shughuli za kitalu nyumba na kufikia dira ya uchumi wa viwanda.
Amesema vijana waunganishwe na mfuko huo ili watafutiwe mashine kwa ajili ya kuweza kuongeza thamani ya mazao kwa kuchakata na kusindika hali itakayofanya vijana wengi wasio na ajira rasmi kujiajiri na kukuza uchumi.
Akiwa Mkoani Shinyanga Mhe. Mavunde ametembelea maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kuweka vitalu nyumba pamoja na vitalu nyumba vilivyopo kwenye Wilaya zote tatu Kishapu, Shinyanga na Kahama.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa