Na. Shinyanga RS.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Solomon Mndeme ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Kahama kwa kuendelea kupata Hati Safi kutokana na ukaguzi za CAG sambamba na kujibu hoja za mwaka 2021/2022.
Mhe. Mndeme ametoa pongezi hizo aliposhiriki katika Kikao Maalumu cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Kahama lililokuwa na ajenda moja kuu ya kupokea na kujadili mapendekezo ya Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambapo Manispaa ya Kahama ilikuwa na Hoja 67 kati ya hizo 48 zilijibiwa na kufungwa wakati 19 zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
“Nawapongeza sana kwa kuendelea kufanya vizuri na kupata hati safi kwa miaka mitano mfululizo, kujibu hoja vizuri na pia nawapongeza sana kwa ushirikiano walionao kati ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita, Waheshimiwa Madiwani, Menejimenti na watumishi wote katika Manispaa umoja ambao unapelekea utendaji kazi kuwa mwepesi na wenye weledi mkubwa kwakuwa pia ndani yake kuna uzalendo,” alisema Mhe. Mndeme.
Kando na pongezi hizo pia aliwaelekeza kutekeleza yafuatayo; kufuatilia na kuhakikisha kuwa wale wote wanaodaiwa na Manispaa wanalipa fedha hizo kwa wakati ili kuzifanya Manispaa kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi wake, kuhakikisha malipo yote yanayofanywa kwa njia ya Mashine za Kukusanyia Mapato (POS) yanapelekwa Benki siku hiyo hiyo yasibakie mikononi mwa wakusanyaji ili kuepusha matumizi ya pesa mbichi.
Maelekezo mengine ni kufuatilia na kuhakiki kuwa hati zote za malipo zinakuwa viambatisho wakati wote na isiwe tu mpaka wakati wa ukaguzi, kuwepo na kitabu cha kumbukumhu kinachoonesha idadi ya Kampuni zote zilizopo Manispaa ya Kahama ili waweze kusimamia ukusanyaji wa ushuruwa huduma kwa wakati kwani kila Kampuni ni lazima kulipia ushuru huo na uwepo wa rejista kwa ajili ya kuhuisha taarifa na kuonesha idadi ya mali za Manispaa.
Picha ikionesha sehemu ya wajumbe waliohudhuria kikao cha baraza maalumu kujadili mapebdekezo ya hoja za CAG katika ukumbi wa Manispaa ya Kahama
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa