Na. Shinyanga RS
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Solomon Mndeme amiziagiza Halmashauri zote Mkoani Shinyanga kuanzisha Dawati na Ofisi Maalumu itakayokuwa na jukumu kuratibu na kushughulikia mambo yote yanayohusu Machinga katika maeneo yao.
Agizo hilo amelitoa leo Julai 22, 2023 wakati akifungua rasmi Kongamano la Shirikisho la Umoja wa Machinga Mkoa wa Shinyanga lililofanyika Wilaya ya Kahama lenye lengo la kumpongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri anayoifanya kwa watanzania wote na hasa Machinga nchi nzima.
Mhe. Mndeme ametoa agizo hilo baada ya kupokea risala ya Shirikisho la Machinga lilisomwa kwake na Mwenyekiti wa SHIUMA TAIFA ndugu Ernest Matondo ambayo ndani yake ilieleza umuhimu wa uwepo wa Dawati na Ofisi Maalumu katika kila Halmashauri ambapo Manispaa ya Kahama wao walikwisha anza kutekeleza mpango huu.
"Nimeskiliza kwa makini lisala yenu, yapo tutakayo yabeba kwenda kuyatekeleza, yapo mengine nayatolea majibu hapa hapa na sasa naagiza kila Halmashauri hapa Mkoani Shinyanga ianzishe haraka Dawati na Ofisi Maalumu itakayokuwa na jukumu la kuratibu na kushughulia mambo ya Machinga peke yake agizo hili lianze kutekelezwa haraka iwezekanavyo," alisema Mhe. Mndeme.
Kando na hayo, pia SHIUMA kwa kauli moja wamesema wanamuunga mkono Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye maamuzi ya Serikali ya Tanzania kuingia mkataba wa uboresha wa utoaji huduma katika Bandari yetu na Serikali ya Dubai na kwamba SHIUMA ipo nae baga kwa bega huku wakimtaka kutowasikiliza hao wasiokuwa na nia njema na Serikali.
Aidha Kongamano hili pia limelenga kupinga mambo yote ya ukatili wa kijinsia na mmomonyoko wa maadili katika jamii zetu, kuhamasisha utunzaji wa mazingira na kupendezesha maeneo yetu kwa faida ya urithi wa Nchi na vizazi vijavyo.
SHIUMA wameipongeza sana Serikali ya Mkoa wa Shinyanga kwa kuwezesha kupatikana kwa suluhu ya machinga ambapo imejenga Soko la Ngokolo (mtumbani), Soko la Ibinzamata, Soko la C. D. T stendi ya Kahama, Soko lq Machinga (mnara wa voda) na soko la mbogamboga Mhunze lililopo Kishapu.
Shirikisho la Umoja wa Machinga (SHIUMA) Tanzania ulipata usajili wake wa awali mwaka 2014 kwa jina la Umoja wa Machinga Tanzania.
Mwaka 2018 Umoja ulianza kuimarika zaidi baada ya kufanya kikao kilichojumuisha Mikoa 14 kwa kushirikiana na OR - TAMISEMI chini ya Waziri Mhe. Jafo S. Jafo, Wizara ya Fedha kupitia Naibu Waziri Mhe. Ashantu Kijaji mkutano ambao ulifanyika Dodoma.
Ilipofika Feb 19, 2019 SHIUMA ilifanya kikao ambacho kilijumuisha Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani na Mei 16, 2022
Picha ikionesha baadhi ya machinga wakiwa kwenye kongamano Kahama-Shinyanga
Mhe. Mndeme akipokea Cheti cha Pongezi kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri ya kuwawezesha machinga katika kutekeleza kazi zao nchi nzima
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa