Na. Shinyanga RS.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Solomon Mndeme na ujumbe wake wametembelea eneo la Viwanda, ambapo wamekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Dubai Textile City, mazungumzo ambayo yamekuwa ni yenye tija sana yaliyoongozwa na Ndg. Mehesh Advani ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Makampuni ya Textile Merchants Group Jijini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.
Kwa niaba ya ujumbe huo, Mhe. Mndeme amewashukuru sana Bodi ya Wakurugenzi kwa ukarimu na ushirikiano wao ambao waliwapatia, hakika wameweza kujifunza mengi mazuri yatakayokuwa na msaada na kuleta ufanisi chanya kwa Mkoa wa Shinyanga na Tanzania kwa ujumla.
Akiongea kwa niaba ya Bodi Ndg. Mehesh pamoja na mambo mengine ameaahidi kuja kutembelea Mkoa wa Shinyanga na kuona namna ambabyo wao WATAWEKEZA katika kukuza uchumi wa wana Shinyanga na kuimarisha uhusiano kati ya Nchi hizi mbili.
Picha ikimuonesha Mhe. Christina Mndeme na baadhi ya ujumbe uliongozana nae katika kutembelea eneo la viwanda.
Mhe. Mndeme akitembelea sehenu ya kiwanda cha Dubai Textile CIty, Abu Dhabi.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa