Na. Paul Kasembo, Kishapu.
NAIBU Waziri wa Maji Mhe. Eng. Mathew Kundo amesema uwepo wa miradi ya maji mingi na mikubwa yenye tija kwa wananchi ambayo inatekelezwa kwa ufanisi mkubwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoani Shinyanga inakusudia kutekeleza nankutafsiri kwa vitendo maono ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya mtua ndoo mama kichwani.
Mhe. Kundo ameyasema haya wakati akikagua utekelezaji wa mradi wa RUWASA wilayani Kishapu ambapo pamejengwa Tangi la maji lenye ujazo wa Lita laki mbili litakaloweza kuhudumia maji safi na salama kwa vijiji 5 zaidi ya wakazi elfu kumi na tano katika Kata ya Uchungai wilayani Kishapu huku akitia wito kwa wananchi kuitunza miundombinu hii muhimu pamoja na vyanzo vya maji.
"Ndugu zangu Wanangundangali hapa Kishapu niwaeleze ukweli kabisa, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewatua ndoo akina mama hapa katika Kata ya Uchunga Kishapu, ambapo kupitia mradi huu wa RUWASA mnaanza kunufaika na maji safi na salama wa vijiji vitano, haya ndiyo maono ya Mhe. Rais wetu kwa wananchi wake na jambo kubwa ni kuhakikisha mnatunza miundombinu hii na vyanzo vyake vya maji," amesema Mhe. Kundo.
Katika hatua nyingine, Mhe. Kundo amempongeza sana Mhandisi Julieth Payovera wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga kwa namna ambavyo anatekeleza kazi zake kwa weledi na ufanisi mkubwa zaidi kwa kushirikiana na wasaidizi wake pamoja na mamlaka nyingine huku akisema utendaji kazi huu ni kilelezo cha uwepo wa watumishi wazalendo na wachapakazi.
Kwa kifupi, ujenzi wa mradi wa Maji ya Bomba Seseko Ngundangalii unatekelezwa na Mkandarasi M/s Otonde Construction and General Supplier wa Mwanza kwa Mkataba No. AE-102/2022/2023/SHY/W/15 chini ya Usimamizi wa RUWASA Wilaya ya Kishapu wakishirikiana na RUWASA mkoa wa Shiyanga. Muda wa utekelezaji ni siku 365 sawa na mwaka mmoja, mradi ulianza kujengwa mnamo tarehe 5/3/2023 na ujenzi wake umekamilika mwezi Juni, 2024.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa