Na.Shinyanga RS.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amewasisitiza watalaamu wa afya kuboresha zaidi utoaji wa huduma kwa wananchi huku akiangazia zaidi katika matumizi ya lugha na kauli zenye staha kwa wananchi sambamba na uhakika wa upatikanaji wa dawa, uhakika wa upatikanaji wa vipimo vya maabara kwa wananchi kwa lugha vipimo kwa kuzingatia taaluma, maadili, viapo, weledi, kanuni na sheria za kitabibu lengo ni kuokoa maisha ya wagonjwa pamoja na kuimarisha utoaji wa huduma kwa watoto wachanga hasa wenye uzito mdogo zaidi waweze kuokolewa huku akisema kwa ujumla Sekta ya afya Kishapu ipo salama kabisa. Mhe. Ummy alisema watumishi wa afya ataendelea kuwakumbusha wajibu na majukumu yao lakini akawataka kutofanya makosa katika taaluma zao jambo ambalo laweza kumpelekea kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria za mabalaza ambapo yaweza kumfutia kibali au leseni yake jambo ambalo asingependa litokee. Ndugu zangu wataalamu wa afya, nipende kuwasisitiza sana katika kuzingatia weledi, maadili, miiko na utu katika utoaji wa huduma kwa wananchi wetu huku tukitumia muda mwingi zaidi kutatua kero na kupunguza malalamiko kwa wananchi wetu na kwa kuhakikisha pia madaktari mnaandika dawa kwa kufuata miongozo ya vitabu vya dawa vya taifa ili kuondoa malalamiko kwa wagonjwa wetu," alisema Mhe. Ummy. Akitoa salamu za Wilaya Mbunge wa kishapu Mhe. Boniphace Butondo alisema kuwa Kishapu kuna upungufu wa watumishi zaidi ya 70% jambo ambalo linazorotesha utoaji wa huduma ukizingatia kuwa kishapu ina jumla ya Kata 29 ambapo Kata zina Vijiji 9 na unakuta kuna watumishi wanne tu na nyumba za watumishi ni chache sana kulingana na mahitaji halisi huku akielezea pia suala la maboma zaidi ya 50 ambayo hayajakamilika. "Mhe. Waziri, kuna suala zima la Zahanati za Kishapu kutokamilika kwa wakati ni kwakuwa Mhe. Mbunge, Madiwani, Mkurugenzi sote tunahamasisha wananchi kuanzisha majengo ya afya ambapo tukiamini kuwa yakifkia hatua flani Serikali itasapoti kukamilisha, sasa kuna maboma zaidi ya 50 hayajakamilishwa , lakini iwapo yangekamilika majengo hayo ni yangesogeza huduma karibu na wananchi wetu," alisema Mhe. Butondo. Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude alisema Hospitali ya Wilaya inakwenda vizuri sana, ambapo kwa sasa wamepokea fedha zaidi ya biloni 2 zilizowezesha kujenga majengo mengi jambo ambalo linapelekea kuongeza na kuboresha huduma zaidi sanjari usimamizi mzuri kwa watumishi. "Tunaendelea kupokea fedha nyingi za dawa, tunasimamia na kudhibiti utoaji wa dawa kwa wananchi, tumeongeza vifaa tiba, majengo na huduma tumeboresha zaidi jambo ambalo linapelekea kuondoa malalamiko kwa wananchi wetu wa Wilaya ya Kishapu," alisema Mhe. Mkude. Pia Mhe. Mkude alisema kuwa suala la maadili na nidhamu kwa watumishi wa Sekta ya afya kishapu limedhibitiwa na sasa hakuna tena tabia hizo mbaya ambazo awali zilikuwa zikiripotiwa kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa na kwamba hakuna malalamiko. Hoja nyingine ilitolewa ni ya upungufu wa gari la wagonjwa (Ambulance) likitajwa kuwa ni muhimu kuongezwa kulingana na ukubwa wa Wilaya ambapo kuna vituo vya afya 8 na vitatu vinakamilishwa hivyo vitakuwa 11 pia kwa kuzingatia jiografia ya Wilaya ilivyo hivyo wakaomba kuongezwa kwa ambulance angalau zifikie ( 3 ) zaidi badala ya moja kama ambavyo tumepangiwa na Serikali hoja ambayo ilijibiwa palepale kwa kupokelewa na Mhe. Waziri alikubaliana na ombi hilo huku akisema zitaletwa ambulance tatu kama walivyoomba. |
MHE. UMMY ASISITIZA UTOAJI WA HUDUMA BORA KWA WANANCHI. Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amewasisitiza watalaamu wa afya kuboresha zaidi utoaji wa huduma kwa wananchi huku akiangazia zaidi katika matumizi ya lugha na kauli zenye staha kwa wananchi sambamba na uhakika wa upatikanaji wa dawa, uhakika wa upatikanaji wa vipimo vya maabara kwa wananchi kwa lugha vipimo kwa kuzingatia taaluma, maadili, viapo, weledi, kanuni na sheria za kitabibu lengo ni kuokoa maisha ya wagonjwa pamoja na kuimarisha utoaji wa huduma kwa watoto wachanga hasa wenye uzito mdogo zaidi waweze kuokolewa huku akisema kwa ujumla Sekta ya afya Kishapu ipo salama kabisa. Mhe. Ummy alisema watumishi wa afya ataendelea kuwakumbusha wajibu na majukumu yao lakini akawataka kutofanya makosa katika taaluma zao jambo ambalo laweza kumpelekea kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria za mabalaza ambapo yaweza kumfutia kibali au leseni yake jambo ambalo asingependa litokee. Ndugu zangu wataalamu wa afya, nipende kuwasisitiza sana katika kuzingatia weledi, maadili, miiko na utu katika utoaji wa huduma kwa wananchi wetu huku tukitumia muda mwingi zaidi kutatua kero na kupunguza malalamiko kwa wananchi wetu na kwa kuhakikisha pia madaktari mnaandika dawa kwa kufuata miongozo ya vitabu vya dawa vya taifa ili kuondoa malalamiko kwa wagonjwa wetu," alisema Mhe. Ummy Akitoa salamu za Wilaya Mbunge wa kishapu Mhe. Boniphace Butondo alisema kuwa Kishapu kuna upungufu wa watumishi zaidi ya 70% jambo ambalo linazorotesha utoaji wa huduma ukizingatia kuwa kishapu ina jumla ya Kata 29 ambapo Kata zina Vijiji 9 na unakuta kuna watumishi wanne tu na nyumba za watumishi ni chache sana kulingana na mahitaji halisi huku akielezea pia suala la maboma zaidi ya 50 ambayo hayajakamilika. "Mhe. Waziri, kuna suala zima la Zahanati za Kishapu kutokamilika kwa wakati ni kwakuwa Mhe. Mbunge, Madiwani, Mkurugenzi sote tunahamasisha wananchi kuanzisha majengo ya afya ambapo tukiamini kuwa yakifkia hatua flani Serikali itasapoti kukamilisha, sasa kuna maboma zaidi ya 50 hayajakamilishwa , lakini iwapo yangekamilika majengo hayo ni yangesogeza huduma karibu na wananchi wetu," alisema Mhe. Butondo. Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude alisema Hospitali ya Wilaya inakwenda vizuri sana, ambapo kwa sasa wamepokea fedha zaidi ya biloni 2 zilizowezesha kujenga majengo mengi jambo ambalo linapelekea kuongeza na kuboresha huduma zaidi sanjari usimamizi mzuri kwa watumishi. "Tunaendelea kupokea fedha nyingi za dawa, tunasimamia na kudhibiti utoaji wa dawa kwa wananchi, tumeongeza vifaa tiba, majengo na huduma tumeboresha zaidi jambo ambalo linapelekea kuondoa malalamiko kwa wananchi wetu wa Wilaya ya Kishapu," alisema Mhe. Mkude. Pia Mhe. Mkude alisema kuwa suala la maadili na nidhamu kwa watumishi wa Sekta ya afya kishapu limedhibitiwa na sasa hakuna tena tabia hizo mbaya ambazo awali zilikuwa zikiripotiwa kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa na kwamba hakuna malalamiko. Hoja nyingine ilitolewa ni ya upungufu wa gari la wagonjwa (Ambulance) likitajwa kuwa ni muhimu kuongezwa kulingana na ukubwa wa Wilaya ambapo kuna vituo vya afya 8 na vitatu vinakamilishwa hivyo vitakuwa 11 pia kwa kuzingatia jiografia ya Wilaya ilivyo hivyo wakaomba kuongezwa kwa ambulance angalau zifikie ( 3 ) zaidi badala ya moja kama ambavyo tumepangiwa na Serikali hoja ambayo ilijibiwa palepale kwa kupokelewa na Mhe. Waziri alikubaliana na ombi hilo huku akisema zitaletwa ambulance tatu kama walivyoomba.
|
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa