Jumla ya miradi 60 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi 15, 305,964,195.75 itapitiwa na Mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani Shinyanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bw. Albert Msovela amesema wakati akipokea Mwenge huo kutoka kwa Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bw. Mohamed Sagini katika kijiji cha Kinampanda kata ya Mwamalasa, Wilaya ya Kishapu, mapema tarehe 10/07/2017.
Miradi itakayofunguliwa, kuzinduliwa, kuwekewa mawe ya msingi na kuonwa imechangiwa na gharama za mfuko wa jimbo, wananchi, Halmashauri, Serikali kuu, wahisani na sekta binafsi.
Mbio za Mwenge wa Uhuru zinaendelea Mkoani Shinyanga ambapo msafara huo utapita katika Wilaya tatu zenye Halmashauri 6 ambazo ni Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu na Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Mwenge wa Uhuru ambao hadi sasa umeshapita katika Halmashauri 3 za Kishapu, Manispaa ya Shinyanga na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, utakabidhiwa kwa Mkoa wa Tabora tarehe 16/07/2017.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa